UGANDA-SIASA

Tume ya Mawasiliano nchini Uganda yaagiza kufungwa kwa mitandao ya kijamii

Mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii ARUN SANKAR / AFP

Tume ya Mawasiliano nchini Uganda, imeagiza kampunin za mitandoa ya Internet kuzima mitandao ya kijamii, siku mbili kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia barua iliyotumwa kwa kampuni zinazotoa huduma hiyo ya Internet, Mkurugenzi Mkuu wa UCC Irene Sewankambo ametaka hatua hiyo kuanza kutekelezwa mara moja.

Hatua hii inamaana kuwa mitandoa ya kijamii kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Signal na Viber itazuiwa na hii inakuja baada ya kampuninya facebook kufunga akaunti za wafuasi kadhaa wa chama tawala NRM.

Kampuni hiyo ya teknolojia imesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuwazuia viongozi wa chama cha NRM, ambao walikuwa wanataka kutumia mtandao huo kuendesha mjadala ambao ungepotosha umma kuelekea uchagusi huo.

Mkuu wa kampuni hiyo barani Afrika, Kezia Anim-Addo, aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, hatua hiyo imechukuliwa ili kuepuka mijadili isiyokuwa na uhalisia nchini Uganda.

Hivi karibuni wafuasi wa NRM walilalamika kutokuwa na uwezo wa kuchapisha taarifa mbalimbali katika mitandao yao, hatua ambayo rais Yoweri Museveni kupitia afisa wake wa Habari Don Wanyama, ambaye pia alifungiwa mitandao yake ,  kusema kuwa hatua hiyo ni mojawapo ya mipango ya nchi za Magharibi kujaribu kjuingilia siasa za nchi hiyo.