UGANDA-UCHAGUZI

Rais Museveni asema aliagiza kufungwa kwa mitandao ya kijamii

Rais wa Uganda  Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. AFP Photo/Marc Hofer

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameituhumu kampuni ya Facebook kwa kuchukua upande kutokana na hatua yake ya kufunga akaunti kadhaa za viongozi na wafuasi wa chama tawala NRM.

Matangazo ya kibiashara

Museveni amethibitisha kuagiza kampuni zinazotoa huduma za Internet nchini humo kufunga mitandao ya kijamii kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi.

Kiongozi huyo aliyekuwa amevalia koti la kijeshi akilihotubia taifa Jumanne usiku, amesema hawezi kuruhu mtu kuichezea nchi hiyo na wale aliosema wanaamua ni chama gani kizuri na kipi kibaya.

Museveni amesema matumizi ya facebook yanastahili kutumiwa kwa usawa na kila mmoja nchini humo.

“Mtandao huo wa kijamii ,iwapo utatumika Uganda ,lazima pawe na usawa, Iwapo unaitenga NRM kwa kuifungia, basi kampuni hiyo haiwezi kufanya kazi Uganda. Mtandao huo wa Facebook, serikali imeifungia ,inasikitisha ila imebidi,”.  amesema.

Carol Korir ripot siasa Uganda Januari 13 2021 I

Siku ya Jumanne, Tume ya Mawasiliano nchini Uganda iliagiza kampuni za mawasiliano nchini humo kufunga mawasiliano katika mitandoa ya kijamii  ya Twitter, WhatsApp, Instagram na  Snapchat .

Hatua hii ya serikali ya Uganda, imelaaniwa vikali na mwanadiplomasia wa Marekani kwa bara la Afrika, Tibor Nagy ambaye kwenye ukurasa wake wa Twitter amesema kianchoendelea nchini humo ni ukiukwaji wa haki za watu.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito kwa wanasiasa na wadau wote wa Uchaguzi huo, kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa utulivu.