UGANDA-UCHAGUZI

Tume ya uchaguzi Uganda yatangaza kumalizika kwa kampeni za uchaguzi

Sanduku la kupiga kura katika uchaguzi uliopita
Sanduku la kupiga kura katika uchaguzi uliopita AFP

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, Jaji Simon Byabakama ametangaza kuwa muda wa kufanya kampeni ya uchaguzi umefikia ukingoni na mtu yeyote hatakiwi kufanya kampeni za namna yeyote ile.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo inakuja siku moja kabla ya uchaguzi, wakati Waganda wanasubiri kuona ni nani atakayeibuka mshindi wa uchaguzi wa urais katika ya wagombea katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na rais anaye maliza muda wake Yoweri Kaguta Museveni, na mpizani wake mkuu Bobi Wine.

Tume ya uchaguzi nchini Uganda imebaini kwamba waandishi wa habari hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura.

Wapigakura zaidi ya Milioni 17 wanatarajia kuamua kati ya wagombea hao yule ambaye atakuwa rais waop mpya.

Wakati huo huo Marekani imelaani kufungwa kwa mitandao ya kijamii nchini Uganda na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametaka kuheshimiwa kwa haki za binadamu kuelekea uchaguzi wa urais nchini humo.

Uganda imeamrisha kufungwa kwa mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na WhatsApp kuelekea uchaguzi wa kesho Alhamisi Januari 14, ambapo rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 anawania muhula wa sita.