UGANDA-MOTOKEO

Kura zinahesabiwa nchini Uganda baada ya wananchi kupiga kura

Kura zinahesabiwa nchini Uganda
Kura zinahesabiwa nchini Uganda Reuters

Kura zimeanza kuhesabiwa nchini Uganda, baada ya mamilioni ya raia nchini humo kupiga kura siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Maeneo mengi ya nchi hiyo vituo vya kupigia kura, vilichelewa kufunguliwa saa moja asubuhi hasa jijini Kampala, licha ya wapiga kura kuwasili mapema.

Mwandishi wa RFI Kiswahili Carol Korir ambaye yupo jijini Kampala, anaripoti kuwa kuna ongezeko la maafisa wa usalama katika maeneo mengi ya jiji hilo.

Malori yaliyojazwa wanajeshi yanaonekana katika barabara kadhaa za jiji hilo, huku hali ya utulivu ikishuhudiwa.

Rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 35 ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 anapambana na wagombea wengine 10 akiwemo mpinzani wake wa karibu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Mtandao wa Internet umezimwa nchini Uganda, pamoja na mitandao ya kijamii.

Mshindi wa uchaguzi wa urais atangazwa siku ya Jumamosi.