UGANDA-MATOKEO

Bobi Wine adai ameshinda urais nchini Uganda, Museveni aongoza

Mgombe wa urais nchini Uganda Bobi Wine kupitia chama cha upinzani NUP akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Januari 15 2021.
Mgombe wa urais nchini Uganda Bobi Wine kupitia chama cha upinzani NUP akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Januari 15 2021. Sumy SADRUNI / AFP

Mgombea wa urais wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amedai kushinda uchaguzi wa urais dhidi ya rais Yoweri Museveni, wakati huu matokeo yakiwa bado yanatangazwa na Tume ya Uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Tayari matokeo yaliyotengazwa na  Tume ya Uchaguzi yanaonesha kuwa Museveni, kiongozi wa muda mrefu nchini humo, anaongoza.

“Nina uhakika kuwa kulimshinda Dikteta kwa mbali. Nawaomba Waganda wote kukataa udanganyifu.Tumeshinda uchaguzi huu, na tumeushinda kwa mbali,” amewaambia wanahabari nyumbani kwake.

“Kinachotangazwa ni wizi mtupu, tunayakataa.”

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Simon Mugenyi Byabakama, amekanusha madai ya Bobi Wine.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa Jumamosi saa 10 jioni.

Ijumaa jioni Bobi Wine, kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika kuwa wanajeshi wamevamia nyumbani kwake.