TANZANIA-CORONA

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania yaonya kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu corona

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA TCRA

Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania TCRA, inaonya kuwachukulia hatua Watu inayosema wanachochea, kuzusha au kupotosha taarifa za corona katika mitandao ya kijamii.

Matangazo ya kibiashara

Tanzania inasema haina virusi cya Corona na tangu mwezi Aprili mwaka uliopita, iliacha kutangaza takwimu za virusi hivyo.

Rais wa nchi hiyo John Magufuli amekuwa akisema nchi hiyo imeponywa na Mwenyezi Mungu na hivyo, Tanzania haina tena maambukizi hayo.

Hivi karibuni, Wiaza ya afya nchini humo, ilitoa utaratibu wa upimaji wa virusi hivyo kwa watu wanaotaka kusafiri nje ya nchi hiyo.

Bei ya kupima maambukizi hayo ni Dola 100 za Marekani, kwa mwenyeji na mgeni.