RWANDA

Visa vya maambukizi vyaongezeka Rwanda

Wanafunzi wakiwa Shuleni nchini Rwanda
Wanafunzi wakiwa Shuleni nchini Rwanda Simon Wohlfahrt / AFP

Wizara ya afya nchini Rwanda imethibitisha kesi mpya mia tano sabini na nne za maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, hii ikiwa ni idadi ya juu kuwahi kushudiwa katika taifa hilo kwa siku moja.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii imeifanya wizara hiyo kuimarisha kampeni zaidi ili kufanya uchunguzi zaidi kwa kila ngazi mitaani, katika kuwahimiza wananchi kukubali kupima Corona kote nchini.

Mwezi Novemba serikali ya Rwanda iilianzisha mkakati wa kupima kwa wingi virusi vya Corona katika shule mbalimbali nchini humo. Wizara za elimu na afya zilipewa jukumu la kusimamia zoezi hilo.

Mpaka sasa watu 181 wameshafariki nchini Rwanda kutokana na ugonjwa wa Corona huku maambukizi yakifikia watu 13,885 na waliopona wakiwa ni watu 8,861.