KENYA - SIASA- KURA YA MAONI

Kenya kushiriki kura ya maoni mwezi June

Kenyan President Uhuru Kenyatta (left) and Opposition leader Raila Odinga shake hands in a show of harmony during the annual prayer breakfast in Nairobi on May 31, 2018
Kenyan President Uhuru Kenyatta (left) and Opposition leader Raila Odinga shake hands in a show of harmony during the annual prayer breakfast in Nairobi on May 31, 2018 Evans Ouma AFP

Raia nchini kenya, wanatarajiwa kushiriki kura ya maoni mwezi june mwaka huu kufanyia katiba marekebisho, kupitia mchakato wa Building Bridges Initiative, maarufu kama (BBI), baada ya mabunge ya serikali za kaunti zaidi ya 24 kupitisha mswaada huo.

Matangazo ya kibiashara

Mswada huo sasa unatarajiwa kuwasilishwa kwa bunge la kitaifa na seneti, ambapo pia unatarajiwa kupata ungwaji mkono ikizingatiwa wabunge wengi na maseneta wanaegemea mirengo ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga, ambao ndio wazilishi wa marekebisho hayo ya katiba.

Tayari kamati ya inayoshughulikia mabadiliko hayo ya katiba inapanga kampeini za taifa zima zitakazoongozwa na rais Kenyatta na Raila Odinga, kupigia debe marekebisho hayo ya katiba.

Hadi kufikia sasa hajabainika wazi iwapo naibu rais wa Kenya, Willam Ruto, ambaye uhusiano wake na rais Kenyatta umeonekana kuyumba siku za hivi karibuni, ataunga mkono marekebisho hayo au la, kwani amekuwa akipinga baadhi ya mapendekezo ndani ya BBI.

Rais Kenyatta ambaye mhula wake unakamilika mwaka ujao, amenukuliwa mara kadhaa akisema, marekebisho hayo yanalenga kuwaunganisha wakenya na wala hatasalia madakani baada kipindi chake kukamilika.