Ufaransa

Christine Lagarde waziri wa fedha wa Ufaransa huenda akamrithi Dominique Strauss Kahn

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Fedha IMF latarajiwa kukutana Ijumaa hii, Mei 20, 2011, mjini Washington kujadili mikakati ya kumrithi Dominique Strauss-Kahn. Tangu kukamatwa kwake Jumamosi Jumamosi iliopita mjini New York jina la Christine Lagarde, Waziri wa Uchumi wa Ufaransalimekuwa likitajwa kama mgombea bora anaefaa kutoka Umoja wa Ulaya.

@Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa fedha wa ufaransa Chritine Lagarde kwa zaidi ya miaka mitatu, ambaye anaongoza rekodi nchini Ufaransa, asifiwa na wenzake wote. Ufahamu wake wa masuala, uwezo wake wa kazi wakati wa mgogoro wa 2008, na kusikiliza katika vikao vya kimataifa, vinasababisha kutambulika. Utendaji wake wa kazi mika ya nyuma unafanya awe kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuchaguliwa.

Kabla ya kuchukua majukumu katika serikali ya Ufaransa, Christine Lagarde alikuwa mwenyekiti wa ofisi ya mahakimu yenye sifa kubwa nchini Marekani. Christine Lagarde anaungwa mkono na mwenziwake wa Sweden, anawezakuwa pia kuwa ni mgombea anaependekezwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Tangu Mei 19, 2011 Gazeti la The New York Times limemueleza kama mgombea bora. Hata hivyo gazeti hilo limetaja na kukumbusha alivyo simamia kesi ya Bernard Tapie / Mkopo wa Credit Lyonnais. Idadi kubwa ya pesa kiasi ya Euro 385,000,000 ilitengwa kwa mahakama ya usuluhishi wa mfanyabiashara ambae alijihisi kuibiwa wakati wa mauzo ya Adidas kwa shirika la mkopo la Credit Lyonnais wakati inayomilikiwa benki.

Christine Lagarde anashutumiwa kuingilia kati na kutatua mgogoro ulioisababisha gharama kubwa kwa taifa. Mahakama yaweza kufanya utafitii katika miezi ijayo kuamua iwapo uamuzi huu ulikuwa halali.

Christine Lagarde atakuwa na kibarua kigumu kuongeza shirika lenye kuhitaji kiongozi mwenye fahamu zaidi na muadilifu katika uongozi wake.