Sudani-kusini

UN yaamrisha jeshi la Sudan kuondoka Abyei

Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah

Umoja wa Mataifa umeitaka Sudan kuondoa vikosi vyake katika jimbo la Abyei baaada ya wanajeshi wa serikali ya Karthoum kuuteka mji wa Abyei. Kitendo ambacho kinachukuliwa kama uvamizi. Wanajeshi wa Sudani Kusini waliondoka katika jimbo hilo l Abyei baada ya mapambano makali yaliosababisha maelfu ya wakaazi wa eneo hilo kuyakimbia makaazi yao. 

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa uliotembelea Sudan mwishoni mwa juma umesema baraza hilo limeingiwa na hofu kutokana na machafuko ya mara kwa mara yanayoripotiwa Abyei.Shirika la kutoa misaada la MSF limesema zaidi ya watu elfu 20 wamekimbia makwao.

Tukio hilo pia limelaaniwa na Umoja wa Ulaya ambao umesema Kitendo cha Sudan kusini kupeleka vikosi vyake Abyei ni tishio kubwa kwa mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2005. Shambulizi hili limetokea wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa ziarani Sudan. Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa linataraji akufanya ziara rasmi Sudani Kusini katika maeneo ya Wau na Juba.

Serikali ya Sudan kusini imesema kitendo hicho cha wanajeshi wa serikali ya Kartoum kuukalia mji wa Abyei ni tangazo la vita.  waziri wa mawasiliano Sudan Kusini Barnaba Marial amelaumu Khartoum kwa kutatua matatizo yake kwa kutumia vujo.
 

Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema mawaziri wa nje wa umoja huo watajadili suala hilo katika kikao chao kitakachofanyika baadae leo mjini Brusseles nchini Ubelgiji.