Uganda, Yoweri Museveni

Wakati wabunge nchini Uganda, wakidai fedha zaidi kuboresha maisha, raia walia

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, akilihutubia taifa.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, akilihutubia taifa. Reuters

Wabunge nchini Uganda wanahitaji kupewa shilingi milioni mia moja sitini kwa lengo la kujiimarisha zaidi ikiwa ni majuma mawili tu, baada ya kuingia bungeni ambapo Baraza jipya la mawaziri lililotajwa likiwa na mawaziri sabini na watano.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imeshazua maswali lukuki huku wachambuzi wa siasa wakiamini wabunge hao, wanaangalia maslahi yao zaidi huku wakiwasahau wananchi ambao wamewapigia kura wakiwa wanahaha kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Makerere na mchambuzi wa Siasa wa siku nyingi Dokta John Nzokwa amewatolea uvivu wabunge hao na kuwataka watambue thamani ya wananchi waliowachagua.

Hatua hiyo inakuja baada ya raia wa Uganda kutumia haki yao msingi, tarehe 18, mwezi Februari mwaka huu, wakati wa uchaguzi mkuu.