Palestina-UN

Katibu mkuu wa UN asema ombi la Palestina kutaka kupewa uanachama linawezekana, litajadiliwa

aps

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa ombi la nchi ya Palestina kutaka kupewa uanachama wa kudumu katika baraza la Umoja wa Mataifa linaeleweka na linawezekana kujadiliwa na kupatiwa uamuzi.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo licha ya kukiri kuwa Palestina ina hoja katika ombi lake ameongeza kuwa ni lazima pande zinazokinzana yani Israel na Palestina wajadiliane kumaliza tofauti zao licha ya kuwa kutakuwa na kura itakayoamua.

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansoor amesema kuwa nchi yake haioni sababu ya kunyimwa nafasi hiyo na kwamba wataendelea kuipigania.

Kikao cha 66 cha baraza la Umoja wa Mataifa kinatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 19 ya mwezi huu ambapo nchi ya palestina inatarajiwa kuwasilisha rasmi ombi lake la kupatiwa uanachama tarehe 23 ya mwezi huu na baadae kupigiwa kura huku nchi za Marekani na Israel zikipinga wazo hilo.