Indonesian

18 Wauwawa katika ajali ya ndege Indonesian

watu wote kumi na wanane waliokuwa kwenye ndege iliyoanguka katika visiwa vya sumatra nchini Indonesia.Kulikuwa na matumaini pengine abiria wangekutwa wakiwa hai baada ya mmoja wa abiria kuelezwa kumpigia simu mama yake akilia baada ya ndege hiyo kupata ajali siku ya Alhamisi.

ajali ya ndege Indonesian
ajali ya ndege Indonesian (REUTERS)
Matangazo ya kibiashara

Baada ya vikosi vya uokoaji kufika eneo la tukio,taarifa ilitolewa kuwa abirio wote waliokuwamo ndani ya ndege hiyo wamepoteza maisha wakiwa wameketi kwenye viti vyao.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Buana liliondoka katika mji wa Medan siku ya alhamisi likielekea karibu na mji wa Aceh lakini baadae lilituma viashiria vya hatari ndege ilipofika katika eneo la milima kaskazini mwa mji wa Medan.