Afghanistan

Kamanda wa juu wa kundi la Taliban amekamatwa Afghanistan

Kamanda wa juu wa kundi la  Haqqani la nchini Afghanistan ambaye pia ni ndugu wa mwanzilishi wa kundi hilo,jalaludin Haqqani amekamatwa. majeshi ya usalama ya NATO yamethibitisha.Tangazo la kukamatwa kwa Haji Mali Khan limekuja baada ya Marekani kuongeza shinikizo kwa serikali ya Pakistan kuchukua hatua dhidi ya mtandao wa Haqqani

Reuters/Ahmad Masood
Matangazo ya kibiashara

Anahusishwa na mashambulizi dhidi ya mataifa ya magharibi.Kahn alikamatwa mjini Paktiya katika mpaka kati ya Afghanistan na Pakistan.Mtandao wa Haqqani umekuwa ukishutumiwa kufanya mashambulizi nchini Afghanistan hasa mjini Kabul,huku hivi karibuni wakishutumiwa kushambulia ofisi za ubalozi wa Marekani ulio mjini humo.