Iran-Marekani

Kiongozi wa kidini nchini Iran aonya kuhusu hatuwa zozote za Marekani dhidi ya nchi yake

Themostimportantnews

Kiongozi wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei ameonya dhidi ya hatua zozote zitakazochukuliwa na nchi ya Marekani kuhusu tuhuma za nchi yake kuhusika na njama za kutaka kumuua balozi wa Saudi Arabia mjini New York kuwa nchi yake haitakaa kimya kujibu.

Matangazo ya kibiashara

Akiongea kupitia televisheni ya taifa Ali khamenei amesema kuwa nchi yake haitakaa kimya kujibu hatua yoyote ambayo itachukuliwa na marekani iwe ya kisiasa au hata kiusalama huku akiendelea kusisitiza nchi yake kutohusika katika mpango huo.

Juma lililopita serikali ya Marekani ilitangaza kuwakamata raia wawili wa Irana wenye ambapo pia wana uraia wa Marekani kwa tuhuma za kukutwa na vitu vya mlipuko pamoja na kupanga njama za kumuua balozi wa saudi Arabia amri ambayo watuhumiwa hao wamedai walipewa kuitekeleza na serikali ya Iran.