UFARANSA

Raia wajitokeza kufanya maamuzi kati ya Francois Hollande na rais Nicolas Sarkozy

europe.chinadaily.com.cn

Raia nchini Ufaransa leo wanapiga kura katika duru la pili la uchaguzi wa rais nchini humo ambapo mpinzani mkuu wa rais Nicolas Sarkozy anayemaliza muda wake, Francois Hollande anamatumaini makubwa ya kupata ushindi katika uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Francois ambaye alimshinda Sarkozy katika duru la kwanza la uchaguzi huo kwa asilimia 27 dhidi ya 26 anaimani kuwa raia wa Ufaransa watamchagua na kumfanya kuwa rais wa kwanza kutoka chama cha soshalisti tangu mwaka 1995

Wapiga kura wapatao milioni 46 wanataraji kupiga kura hii leo katika vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini humo baada ya kukamilika kwa kampeni siku ya Ijumaa.