SUDANI

Sudani yasema inaona ugumu katika kutekeleza azimio la umoja wa mataifa UN

in2eastafrica.net

Sudan imesema kuwa huenda kukawa na ugumu katika kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa ambao una lengo la kukomesha majuma kadhaa ya mapigano mpaka na kutatua masuala muhimu baina yake na Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya kigeni nchini humo imesema kuwa imethibitisha kwa maandishi katika baraza la usalama la umoja wa Mataifa UN na Umoja wa Afrika kuhusu dhamira yake ya kukomesha uhasama katiyake na Sudani Kusini,chini ya azimio lililopitishwa siku ya Jumatano.

Hata hivyo Sudani imeelezea kutokuridhishwa kwake na baadhi ya mambo ambayo huenda yakasababisha ugumu katika kutekeleza kikamilifu azimio hilo.