Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Jeshi la Uganda lamkamata mmoja wa viongozi wa Kundi la LRA Meja Acellam huku Umoja wa Mataifa UN ukisema Al Qaeda imeweka mizizi Syria
Imechapishwa:
Cheza - 19:42
Jeshi la Uganda limefanikiwa kumkamata Mmoja wa Viongozi wa Kundi la Waasi la LRA Meja Caesar Acellam, Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC yaendelea kumsaka Mbabe wa Kivita Jenerali Bosco Ntaganda, Utata waanza kugubika serikali ya Mali baada ya madai ya kukiukwa kwa katiba kuanza kujitokeza, Umoja wa Mataifa UN wasema mashambulizi yanayofanyika nchini Syria kwa sasa yanamkono wa Mtandao wa Kigaidi wa Al Qaeda na Marekani yaanza kuchukua hatua kuhakikisha soko la hisa la Wall Streets halikumbwi na misukosuko.