Baada ya mkutano wa Bagdad Iran na mataifa tajiri kukutana jijini Moscow
Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani yamefanikiwa kwa kiasi kidogo katika mkutano wao wa siku mbili juu ya maswala ya Nuklia Mazungumzo yaliyofanyika mjini Baghdad nchini Iraq.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mataifa hayo yamekubaliana kukutana tena jijini Moscow nchini Urusi tarehe 18 na 19 mwezi ujao ili kuendelea na mazungumzo yao.
Mkuu wa Sera za kigeni ndani ya Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton amesema kuwa wanaendelea kuwa na imani kuwa wataweza kufikia muafaka siku za karibuni kupitia mazungumzo, na kuahidi kuwa watafanya juhudi mpaka mwisho.
Hatahivyo ametanabaisha kuwepo kwa hali ya kutokubaliana na kuitaka Iran kutekeleza hatua zilizopendekezwa na Jumuia ya kimataifa.
Ashton aliweka mapendekezo mapya mezani kwa niaba ya mataifa hayo, Mapendekezo ambayo hayakuridhiwa na Iran
Mataifa hayo yametaka Irana kupunguza mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium kwa asilimia 20, mpango ambao mataifa hayo yamehofu kuwa Iran inampango wa kutengeneza silaha za hatari.