MISRI

Chama cha udugu wa kiislam chawaomba wamisri kumuunga mkono mgombea wake katika duru la pili la uchaguzi.

Chama cha udugu wa kiislam cha nchini Misri, Muslim Brotherhood, kimewataka Wamisri kumuunga mkono mgombea wao wa urais katika duru la pili la uchaguzi dhidi ya mpinzani wake Ahmed Shafiq, kikionya kwamba nchi itakuwa hatarini endapo aliyekuwa waziri mkuu katika kipindi cha utawala wa kiimla wa rais Hosni Mubarak atashinda.

Wagombea wa urais nchini Misri
Wagombea wa urais nchini Misri viewtz.com
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Muslim brotherhood jana Ijumaa kilitangaza kuwa mgombea wake Mohammed Mursi anaongoza katika uchaguzi uliofanywa May 23 na 24 baada ya kura zote kuhesabiwa huku mpinzani wake Ahmed Shafiq akifuatia katika nafasi ya pili.

Hatua ya kurudiwa kwa uchaguzi kati ya Shafiq na Mursi itazidi kuligawa taifa hilo ambalo raia wake walisimama kupinga utawala wa mabavu wa rais Hosni Mubarak miezi 15 iliyopita lakini tangu wakati huo linakabiliwa na vurugu na kushuka kwa uchumi.

Tume ya uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo rasmi siku ya Jumanne.