Habari RFI-Ki

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yakataa kufanya mazungumzo na Kundi la Waasi la M23

Sauti 09:33
Maelfu ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakikimbia mapigano yanaendelea kuchacha Mashariki mwa nchi hiyo
Maelfu ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakikimbia mapigano yanaendelea kuchacha Mashariki mwa nchi hiyo

Makala ya Habari Rafiki itamulika mwendelezo wa Mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC ambapo Jeshi la serikali limeamua kuwasambaratisha wapiganaji waasi wa Kundi la M23 ambao wengi wao ni askari watiifu kwa Jenerali Bosco Ntaganda anayesakwa kama lulu na Mahakama ya ICC.Mapigano hayo yamechukua sura mpya,wakati wapiganaji hao wameiomba serikali ya DRC kuandaa mazungumzo kitu kilichopingwa na serikali.