Habari RFI-Ki

Siku ya Tumbaku yaadhimishwa huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka kwa magonjwa yanayotokana na kuvuta sigara

Sauti 09:54
Sigara ni bidhaa ambayo inatengenezwa kwa kutumia tumbaku na watumiaji wake wanafahamu madhara yanatopatikana kwa kuvuta
Sigara ni bidhaa ambayo inatengenezwa kwa kutumia tumbaku na watumiaji wake wanafahamu madhara yanatopatikana kwa kuvuta

Tarehe 31 Mei ni siku ya Tumbaku Ulimwenguni. Na kauli mbiu yake mwaka huu ni: "Kutokuwa na Tumbaku Ulimwenguni" Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO inaonyesha kuwa watu laki sita hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa yanayotokana na uvutaji wa sigara, wakati watu elfu kumi na tatu wanakufa kwa siku na watu sita kwa kila sekunde. Nchini Uganda,Wizara ya afya imethibitisha kuwa mswada umeandaliwa na sasa upo tayari kuwasilishwa Bungeni ili kupiga marufuku Upandaji wa Tumbaku na Uvutaji wake.