Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Serikali yalaani machafuko Visiwani Zanzibar na Umoja wa Mataifa UN yataka Somalia ipatiwe msaada wa kujijenga

Sauti 16:29
Waandamanaji Visiwani Zanzibar wanaoshinikiza kuvunjika kwa Muungano wa Tanzania wakionesha hisia zao kwa njia ya maandamano
Waandamanaji Visiwani Zanzibar wanaoshinikiza kuvunjika kwa Muungano wa Tanzania wakionesha hisia zao kwa njia ya maandamano

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imelaani machafuko yaliyoratibiwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar JUMIKI yaliyozusha ghasia na kuchangia kuharibiwa kwa mali mbalimbali, Umoja wa Mataifa UN watoa wito kwa mataifa rafiki kwa Somalia na Jumuiya ya Kimataifa kuisadia nchi hiyo iweze kujijenga upya na hofu ya kuibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria imezidi kugubika nchi hiyo huku Urusi ikilaumiwa kuuza silaha kwa serikali ya Rais Bashar Al Assad.