Marekani-China

Marekani yataka Uchina kuwaachilia mamia ya wanaharati wa Tianenmen.

Wa Chiina waandamana
Wa Chiina waandamana REUTERS/David Gray

Mamia ya wanaharakati wamekusanyika mjini Beijing nchini China, kuadhimisha miaka 23 tangu kukamatwa na kuzuiliwa kwa mamia ya wanaharakati waliokuwa wanaandamana katika eneo la Tianenmen.

Matangazo ya kibiashara

Marekani inataka Beijing kuwaachilia huru mamia wa wanaharakati ambao bado wanazuilia kwa sababu ya kuandamana mwaka 1989,kupinga visa vya ukiukwaji wa haki za kibinadamu na ufisadi nchini humo.

Pamoja na kuzuiliwa mamia ya watu waliuawa mikononi mwa maafisa wa polisi kwa kupigwa risasi wakati wakifanya maandamano hayo ya amani.

Serikali ya China inazuia maadhimisho hayo kufanyika na polisi wameonekana katika kona mbalimbali mjini Beijing wakiwa wamejitahami kukabiliana na watu watakaojitokeza katika maadhimisho hayo.

Waandalaizi wa maadhimisho hayo wanasema wanatarajiwa zaidi ya watu laki moja kuhudhuria maadhimisho hayo.

Beijing imeendelea kushutumiwa kwa kuminya haki za bindamu na kuwanyanaysasa wanaharakati wanaokosoa serikali.