Urusi-Umoja wa Ulaya

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kukutana jijin Saint Petersbourg kuzungumzia mzozo wa Syria

Jose Manuel Barroso mkuu wa tume ya  Umoja wa Ulaya
Jose Manuel Barroso mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya Reuters/Sebastien Pirlet

Viongozi wa Ulaya, wanakutana mjini Saint Petersburg nchini Urusi kuzungumzia maswala ya umoja huku, katika mkutano huo ukitarajia kutawaliwa na mjadala kuhusu machafuko yanayoendelea nchini Syria. Maafisa hao wanatarajiwa kumshinikiza rais Vladimir Putin kubadilisha sera yake kuhusu machafuko yanayoendelea nchini Syria,ambayo yamesababisha mauji ya maelfu ya watu.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa EU,wanataka kutumia Urusi kama ngazi za kushinikiza kuondolewa kwa silaha hatari na wanajeshi wa wa serikali katika ngome ya wapinzani na mpango wa amani ulioundwa na mjumbe wa Umoja wa matifa Koffi Annan kuzingatiwa.

Urusi na Uchina zimeenedelea kutumia kura zao za veto kupinga azimio lolote dhidi ya rais wa Syria Bashar Al Assad na washirika wake,kama inavyoshinikizwa na Marekani na mataifa mengine ya umoja wa Ulaya.

Siku ya jumapili rais Assad alikansuha serikali yake kuhusika na mauji ya kinyama yaliyotokea katika mji wa Houla wiki iliyopita baada ya kuuliwa kwa watu zaidi ya 100 wakiwemo watoto na wanawake.

Serikali ya Syria imeiimbikizia lawama wapinzani kwa kutekeleza mauaji hayo,tuhma wapinzani wamepinga .

Umoja wa Mataifa unasema msimamo wa Urusi dhidi ya Syria unachangia kwa machafuko hayo kuendelea zadi, na inaonya kuwa Syria inaelekea katika vuta vya wenyewe kwa wenyewe.