PAKISTAN

Abu Yahya al-Libi naibu kiongozi wa al-Qaeda anaripotiwa kuuawa nchini Pakistan

Marekani inasema shambulizi  lililofanywa na ndege zake za kivita zisizokuwa na rubani nchini Pakistan limesababisha kuuawa kwa Abu Yahya al-Libi, naibu kiongozi wa kundi la al Qaeda. 

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lilitokea karibu na mpaka wa Afganistan na haijafamika vema ikiwa al-Libi, alikuwa miongoni mwa washukiwa 15 wa al-Qaeda waliouawa katika shambulizi hilo.

Shambulizi hilo limekashifiwa vikali na serikali ya Pakistan ambayo imekuwa ikiendelea kukashifu mashambulizi hayo yanayofanywa na Marekani,kwa kile inayosema kuwa mashambulizi hayo yamewauwa  raia wasiokuwa na hatia.

Uchunguzi unaendelea kubaini ikiwa kweli al Libi aliuawa katika shambaulizi hilo au la na ikiwa ni kweli,itakuwa ni pigo kubwa sana kwa kundi hilo la al qeda ambalo limeendelea kutishia usalama wa dunia.

Maafisa wa usalama mjini Peshawar nchini Pakistan wanasema kuwa huenda kiongozi huyo ameualiwa madai ambayo hayajathibitishwa rasmi na vyombo vya kitaifa vya usalama mjini Islamabad.

Al Libi amekuwa akitafutwa tangu mwaka 2009,na mwaka huo aliripotiwa kuuawa taarifa ambazo zilikanushwa baadaye.

Marekani inaamini kuwa kuuawa kwa Osama Bin Laden,mwaka uliopita sasa Libi ndiye wa pili katika uongozi wa al qaeda baada ya Ayman al Zawahiri raia wa Misri kuchukua uongozi wa kundi hilo.

Libi anaripotiwa kuwa msimamizi wa oparesheni za kila siku nchini Pakistan.