SYRIA

Syria yakubali misaada ya kibinadamu kutoka masharika ya kimataifa

Umoja wa Mataifa unasema serikali ya Syria imekubali kuingia kwa misaada ya kibinadamu kutoka kwa mashirika ya kimataifa kuwafikia waathiriwa wa machafuko yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Itakuwa mara ya kwanza kwa mashirika ya kimataifa kuleta misaada yao nchini humo,na kuungana na shirika la kimtaifa la msalaba mwekundu ambalo limekuwa likiendela kutoa misaada mbalimabli katika miji iliyaothiriwa zaidi ya Homs, Idlib na Deir Azzor.

Mkurugenzi Mkuu anayesdhughulikia maswala ya dharura katika Umoja wa Mataifa, John Ging amesema tayari maafisa wake wametumwa katika maeneo mbalimbali kuthamini kiwanngo cha msaada kinachohitajika.

Mbali na hayo, Damascus imewazuia mabalozi 17 kuingia Syria kutoka kwa mataifa yao kuendelea kupinga uongozi wa rais Bashar al Assad.

Miongoni mwa mabalozi ambao wamepigwa marufuku kuingia nchini Syria ni pamoja na wale kutoka Marekani, Uingereza na Uturuki mataifa ambayo yamekuwa katika mstari wa mbele kupinga uongozi wa rais Assad.

Mawaziri kutoka Mataifa 30 akiwemo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton wanatarajiwa kukutana kesho mjini Instabul nchini Uturuki kujadiliana na kutafuta namna ya kumaliza machafuko nchini Syria.

Rais Bashar Al Assad ameshtumiwa na mataifa ya Magharibi kwa kukataa kutekeleza mpango wa amani ulioandaliwa na msuluhishi wa kimataifa wa mgogoro huo Koffi Annan.