SYRIA

Majeshi ya Syria yawazuia waangalizi wa Umoja wa Mataifa kuzuru katika eneo la mauji

Majeshi ya serikali ya Syria yamewazuia waangalizi wa Umoja wa Mataifa kuzuru katika eneo ambalo watu 55 wengi wao wakiwa watoto na wanawake waliouliwa mjini Hama. 

Matangazo ya kibiashara

Kuzuiliwa kwa waangalizi hao kumethibitihswa na kiongozi wao Jenerali Robert Mood ambaye amesema waangalizi hao walikwenda kuthibitisha kuhusu mauji hayo,na kuthathmini namna yalivyotokea na kukumbana na wanajeshi wa serikali waliowazuia kufika katika eneo hilo.

Kwa upande mwingine, shinikizo zinatolewa kwa rais Bashar Al Assad kujiuzulu kutokana na mauaji hayo ambayo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanailaumu serikali ya rais Assad kuvihami vikundi vya watu kuvamia ngome ya wapinzani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema rais Assad ni lazima ajiuzulu na kuondoka nchini Syria mara moja, kwa kuendelea kuwaua raia wake kutumia makundi ya watu waliojihami kwa silaha.

Clinton ameongeza kuwa mauji hayo hayawezi kuendelea na kuonya kuwa ni sharti mataifa ya Urusi na Uchina yanayopinga Umoja wa Mataifa kuichukulia Syria hatua kubadilisha msimamo wao.

Mauji haya yanatokea wiki moja tu baada ya kutokea kwa mauji mengine kama haya katika mji wa Houla ambapo watu 108 waliuawa mikokoni mwa kundi lingine la watu waliojihami.

Serikali jijini Damascus imesema,  mauaji haya yametekelezwa na magaidi na imekanusha  tuhma kuwa inafadhili makundi ya watu kutekeleza mauji hayo katika ngome za wapinzani.

Baraza la upinzani nchini Syria linasisitiza kuwa mauaji yanayotokea yanafanywa na kundi linalofahamika kama shabiha ambalo limefadhiliwa na serikali na linamuunga mkono rais Bashar Al Assad.

Mataifa ya Magharibi yanakashifu serikali ya Syria kutekeleza mauaji hayo na inamtaka rais Assad kujiuzulu na imewafukuza Mabalozi wa Syria katika nchi zao.

Hata hivyo, mataifa ya Uchina na Urusi yameendelea kupinga uwezekano wa Syria kuingiliwa kijeshi na zimeapa kutumia kura zao za veto kupinga azimio lolote dhidi ya serikali ya rais Bashar Al Assad.

Msuluhishi wa kimataifa wa mgogoro huu  Koffi Annan anatarajiwa kuwahotubia wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu machafuko hayo.

Maelfu ya watu wameuawa nchini Syria kwa kipindi cha miezi 15 iliyopita