SYRIA

Waangalizi wa umoja wa mataifa washuhudia damu na harufu ya miili iliyochomwa moto kijijini Al Kubeir

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Martin Nesirky
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Martin Nesirky unmultimedia.org

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao walikwenda katika kijiji cha Al-Kubeir yalikotokea mauaji ya kinyama nchini Syria wamesema wameona damu juu ya kuta na wakahisi harufu ya mwili kuteketezwa lakini hawakuweza kuthibitisha idadi ya waliouwawa.

Matangazo ya kibiashara

Wakati serikali ikikanusha kuhusika na mauaji hayo,msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky amesema kuwa waangalizi wameshuhudia magari ya kivita katika maeneo ya kijiji hicho, nyumba zilizoharibiwa na makombora, mabomu na silaha mbalimbali.

Takribani watu 55 waliuawa siku ya Jumatano katika shambulizi kijijini Al-Kubeir katika jimbo la Hama, kwa mujibu wa taasisi ya waangalizi wa haki za binadamu ya nchini Syria.