Syria

Kiongozi mpya wa baraza la upinzani awataka wananchi wa Syria kujitokeza kwa wingi kuupinga utawala wa Bashar Al Assad

Abdel Basset Sayda kiongozi mpya wa upinani nchini Syria
Abdel Basset Sayda kiongozi mpya wa upinani nchini Syria REUTERS/Osman Orsal

Uongozi mpya wa baraza la upinzani nchini Syria unataka raia wote nchini humo kujitokeze na kuishtumu serikiali ya rais Bashar Al-Assad. Abdelbaset Sayda alichaguliwa kuchukua nafasi iliochwa wazi na Burhan Ghalioun, aliyeshikilia wadhifa huo tangu kundi hilo liundwe mnamo mwezi Septemba na ambae alijiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Wito kama huo pia unatolewa na jeshi huru nchini humo linalopambana na wanajeshi wa serilkali ambalo sasa pia linasema wakati umefika kwa raia wote wa syria kujitokeza barabarabi na kuendelea na maandamano.

Abdel Basset Sayda kiongozi mpya wa baraza hilo la upinzani amesema mauji nchini mwake lazima yakome na serikali kuheshimu matakwa ya wananchi nchini humo, badala ya kuwaua.

wakati hayo yakiarifiwa, mapambano makali yanaendelea kushuhudiwa nchini humo baina ya vikosi vya serikali ya rais Bashar Al Assad na wapiganaji wa jeshi huru la Syria ambao walifaulu kushambulia msafara wa bus la wafanyakazi wa mafuta kutoka nchini Urusi jiji Damascus.

Wengi wa waasi hao wa jeshi huru la Syria waliohusika katika mashambulizi tofauti waliauwa.

wakati huohuo makam waziri mkuu wa Israel Shaul Mofaz, ameituhumu serikali ya rais Bashar Al Assad kutekeleza mauaji ya kimbari dhidhi ya raia wake wanaodai mabadiliko miezi kumi na tano sasa.

Shaul Mofaz amesema kwamba jamii ya kimataifa imeshindwa kukomesha mauaji yanayoendelea kutekelezwa na rais Bashar Al Assad.