Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania atekwa wakati huu ambapo Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Syria ikipendekezwa
Imechapishwa: Imehaririwa:
Sauti 21:44
Mgomo usio na kikomo nchini Tanzania waanza huku Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dokta Ulimboka Steven akitekwa na kupigwa vibaya, Wahamiaji 43 kutoka Ethiopia wapoteza maisha na miili yao kutekelezwa nchini Tanzania, Rwanda yaituhumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa kufadhili waasi wa FDLR, Kofi Annan atoa pendekezo la kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa na mdororo wa uchumi kwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya EU waendelea huku suluhu ikisakwa.