SYRIA

Ufaransa kuongoza kikao kuhusu Syria, wakati watu laki mbili wakikimbia mashambulizi katika mji wa Aleppo

Ufaransa inapanga kuandaa kikao cha dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria pindi itakapochukua uongozi wa baraza hilo mwezi ujao wa nane. Takriban watu laki mbili wamelazimika kuutoroka mji wa Aleppo na kukimbilia nchini Uturuki

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Ufarasa Laurent Fabius amesema mkutano huo utaokahudhuriwa pia na Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazowakilishwa katika baraza hilo utatafuta mbinu za kuhakikisha kuwa rais Bashar Al Assad anasitisha mashambulizi dhidi ya wapinzani.

Mashambulizi ya wanajeshi wa Syria dhidi ya wapiganaji wa upinzani katika jijini la Allepo limesabaisha watu Laki mbili kutoroka makwao katika kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Uogozi wa upinzani unalaumu serikali kwa kupanga mauji dhidi ya raia wasiokuwa na hatia katika mji huo kwa kutumia silaha hatari pamoja na ndege za kijeshi, mashambulizi ambayo yameendelea kushtumiwa na mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani ambayo inasema siku za rais Assad kusalia uongozini zinahesabiwa.

Serikali jijini Damascus kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje Walid al-Muallem, akiwa nchini Iran amesema kuwa jeshi la serikali haliwalengi raia bali linawatafuta magaidi.

Abdel Basset Sayda kiongozi wa baraza la upinzani anazuru Iraq siku ya Jumatatu kuzungumza na viongozi wa serikali hiyo kutafuta uungwaji mkono katika harati zake za kuikomboa Syria.

Zaidi ya watu elfu 20 wameuawa kutokana na machafuko hayo yaliyoanza mwaka uliopita.

Upinzani nchini Syria unataka uongozi wa rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani.