Urusi

Rufaa ya wanamuziki waliofungwa jela kwa kukashifu utawala wa rais Putin yaahirishwa

Mahakama nchini Urusi imeahirisha kusikiliza rufaa ya wanamuziki wa Roki, Pussy Riot ambao awali walihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela makosa ya kukashifu utawala wa rais Putin kanisani.

Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo sasa itasikilizwa tarehe 10 mwezi huu, baada ya mmoja ya Yekaterina Samutsevich mmoja wa wanamuziki hao kudai kuwa wametofautiana kuhusu kesi hiyo na wakili wake wa kwanza.

Wanamuziki hao watatu kabla ya kuhukumiwa mwezi Agosti mwaka huu walikuwa kizuizini kutoka mwezi wa Machi ambapo upinzani pamoja na wanaharakati wa demokrasia na haki za binadamu Aung San Suu-Kyi wamekosoa hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo.

Kwa mujibu wa wanasheria wa wanamuziki hao, wamesema kuwa hawatarajii kuona mabadiliko makubwa kwenye hukumu ya awali ingawa wanamatumaini kuwa kifungo chao huenda kikapungua na kufikia nusu mwaka.