Iran

Iran kuendelea na mpango wake wa Nuclear licha ya changamoto za kiuchumi

Iran inasema haitasitisha mpango wake wa nuclear licha ya changamoto za kiuchumi inayopitia kwa sasa kutokana na vikwazo vya kiuchumi  kutoka kwa mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Rais Mahmoud Ahmadinejad amesema licha ya sarafu ya nchi hiyo kushuka thamani kwa kiasi kikubwa, serikali yake haitatishika na vikwazo hivyo na badala yake itaendelea na mpango huo ambao ameendelea kusema ni wa amani.

Aidha, Ahmadinejad ameongeza kuwa tabia ya nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kuendelea kuishinikiza kuachana na mpango huo inastahili ikomee kwa kile alichokieleza kuwa hawawezi kamwe kuwaamulia watu Iran jambo la kufanya.

Sarafu ya Iran rial, kwa sasa imepungua thamani yake kwa asilimia 80 ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita baada ya mapema wiki hii kushuka kwa asilimia 17, jambo ambalo Tehran inasema ni vita vya kiuchumi kutoka Marekani.

Marekani inasema kutetereka kwa sarafu ya Tehran ni wazi kuwa vikwazo dhidi yake vinafanya kazi na raia wa nchi wa nchi hiyo wanafahamu chanzo cha mgogoro huo wa kiuchumi ni viongozi wao.

Marekani ikiongoza mataifa ya Magharibi inashinikiza Iran kuachana na mpango wake wa Nuclear kwa kurubisha madini ya Uranium yanayoshukiwa kutengeneza silaha za maangamizi.

Israel imeendelea kusisitiza kuwa mpango wa Iran unawalenga wao moja kwa moja na kutaka Mataifa ya Magharibi kuiwekea serikali ya Iran muda wa mwisho wa kuachana na mpango huo.