Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Majeshi ya AMISOM yaendelea kuimarisha usalama Kismayo huku Syria na Uturuki zikiwa hatarini kuingia vitani

Sauti 19:12
Jeshi la Kenya likiwa chini ya mwanvuli wa AMISOM wakifanya doria katika Mji wa Kismayo baada ya kuwasambaratisha Wanamgambo wa Al Shabab
Jeshi la Kenya likiwa chini ya mwanvuli wa AMISOM wakifanya doria katika Mji wa Kismayo baada ya kuwasambaratisha Wanamgambo wa Al Shabab

Majeshi ya Kenya KDF yakiwa chini ya mwamvuli wa Vikosi vya Umoja wa Afrika Vinavyolinda Amani nchini Somalia AMISOM yanaendelea na operesheni zao kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika Mji wa Kismayo baada ya kuwasambaratisha Wanamgmbo wa Al Shabab, Wanajeshi wanne raia wa Nigeria ambao wapo kwenye Vikosi vya Kulinda Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan UNAMID wamepoteza maisha kwenye shambulizi lililotekelezwa na watu wenye silaha, Syria na Uturuki zipo kwenye hatari ya kuingia kwenye vita hatua ambayo imekuja siku chache baada ya kutokea kwa vifo vya watu watano huko Istanbul kufuatilia shambulizi lililofanywa na Majeshi ya Damascus na kwa mara ya kwanza Wagombea wawili wa urais nchini Marekani Rais Barack Obama na Mitt Romney kwa mara ya kwanza wamepambana kwenye mdahalo wa Televisheni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.