Kutetereka kwa Uhusiano baina ya Vyombo ya Usalama na Raia katika nchi za Afrika Mashariki

Sauti 09:55
Jeshi la Polisi nchini Tanzania likipambana na Waandamanaji
Jeshi la Polisi nchini Tanzania likipambana na Waandamanaji

Makala ya Habari Rafiki yanaangazia suala la mahusiano baina vyombo vya usalama katika nchi za Afrika Mashariki na raia wake. Suala hili linakuja kufuatia matukio ya hivi karibuni kushuhudia raia wakipoteza maisha mikononi mwa vyombo vya usalama lakini pia kushambuliwa na kuuawa kwa askari polisi. Wasikilizaji wanapaza sauti zao kutathmini mahusiano hayo na kuyatolea maoni yanayoweza kuleta ufumbuzi.