Habari RFI-Ki

Serikali ya Tanzania yaridhia ombi la wafanyakazi na wabunge la uwepo wa fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii

Sauti 10:01
Wabunge nchini Tanzania wakiwa Bungeni wao walikuwa ni miongoni mwa wale walioshinikiza kuruhusiwa uwepo wa fao la kujitoa kwenye mashirika ya hifadhi za jamii
Wabunge nchini Tanzania wakiwa Bungeni wao walikuwa ni miongoni mwa wale walioshinikiza kuruhusiwa uwepo wa fao la kujitoa kwenye mashirika ya hifadhi za jamii

Baada ya wafanyakazi na baadhi ya wabunge nchini Tanzania kusema heri kufa macho kuliko kufa moyo na kuilalamikia sheria ya jamii ya mwaka 2012 inayozuia mwanachama kujitoa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii. Jitihada zao zimezaa matunda baada ya serikali kuridhia wafanyakazi kujitoa kwenye mifuko hiyo na kupewa mafao yao kama ilivyokuwa awali.