UFILIPINO

Hali ya sintofahamu yaendelea kutanda nchini Ufilipino kufuatia kimbunga cha

Wananchi wa Ufilipino wakijaribu kuondoa mti ulioanguka barabarani baada ya kimbunga cha Bopha
Wananchi wa Ufilipino wakijaribu kuondoa mti ulioanguka barabarani baada ya kimbunga cha Bopha Reuters

Zaidi ya wananchi elfu 40 wameyakimbia makazi nchini Ufilipino kufuatia nchi hiyo kukumbwa na kimbunga cha Bopha ambacho kimesababisha mafuriko yaliyoleta uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Matangazo ya kibiashara

Kimbunga hicho kimeshuhudia kiking'oa miti mikubwa na kuharibu miundombinu ya barabara na umeme na kusababisha hali ya taharuki kwa wananchi ambao wamekuwa wakikimbia kunusuru maisha yao.

Kimbunga cha Bopha kimeelezwa kuwa kibaya zaidi kuikumba nchi ya Ufilipino kwa mwaka huu ambapo serikali imewataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya mabondeni kuyahama makazi yao.

Kwa mujibu wa kitengo cha maafa nchini humo wamesema kuwa maeneo yaliyoathirika ni kwenye visiwa vya Mindanao na sasa kimekuwa tishio kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Manila.

Mpaka sasa ni mtu mmoja tu ndio hajulikani alipo inagwa vikosi vya uokoaji vinadai kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka kutokana na kuripotiwa madhara makubwa kwenye baadhi ya maeneo huku familia kadhaa zikiripoti ndugu zao kupotea.

Mpaka sasa huduma za usafiri wa anga zimesitishwa kwa muda huku shule nyingi nazo zikitangazwa kufungwa kupisha kimbunga hicho ambacho kinaelezwa kitaikumba nchi hiyo kwa siku kadhaa.