SYRIA-DAMASCUS

Mlipuko wa bomu la kujitoa muhanga waua watu 30 mjini Damascus, Syria

Moja ya matukio ya ulipuaji wa mabomu yaliyotekelezwa hivi karibuni mjini Damascus
Moja ya matukio ya ulipuaji wa mabomu yaliyotekelezwa hivi karibuni mjini Damascus REUTERS

Mlipuko wa bomu la kujitoa muhanga kwenye mji wa Damascus nchini Syria umeelezwa kusababisha vifo vya watu 30 na kujeruhi wengine zaidi ya hamsini . 

Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kutetea haki za binadamu mjini Damascus yamethibitisha kutokea kwa mlipuko huo na kwamba mtu mmoja aliyekuwa kwenye alijitoa muhanga nje ya jengo ambalo hutumiwa na wapiganaji ambao wanauunga mkono utawala wa rais Bashar al-Asad.

Shambulizi hilo linatokea wakati ambapo juhudi za Umoja wa nchi za Kiarabu kujaribu kumaliza mzozo unaendelea nchini humo zikigonga mwamba na kushindwa hata kutoa tumaini la kumaliza machafuko nchini humo.

Hivi karibuni Umoja wa Nchi za Kiarabu uliingilia kati tena mgogoro wa Syria kwa kuzitaka pande zinazokinzana nchini humo kuketi meza moja, wito ambao ulipuuziliwa mbali na Serikali ya rais Asad.

Serikali mjini Damascus imekuwa ikiwatuhumu viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu kwakuwa vibaraka wa nchi za magharibi na kwamba wao ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha kuendelea kushuhudiwa machafuko nchini humo.

Wakati huohuo Umoja wa Mataifa umesema kuwa utaendesha uchunguzi wake kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria yakiwemo mauaji ya halaiki ambayo yanatekelezwa na pande zote mbili zinazopigana nchini humo.

Katika hatua nyingine Serikali ya Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa Serikali ya rais Asad imetangaza kutuma ndege mbili nchini Lebanon kuwaondoa rais wake zaidi ya 100 ambao bado wako nchini Syria.