DRC-UGANDA-M23

Waasi wa M23 wamtaka rais Museven kuingilia kati mazungumzo yao na Serikali ya Kinshasa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Joseph Kabila REUTERS/Edward Echwalu

Kundi la Waasi la M23 linalopambana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika eneo la Mashariki limetaka Rais wa Uganda ambaye ni Mkuu wa Nchi za Maziwa Makuu ICGLR kuingilia kati ili kupata suluhu ya mvutano uliopo kwa sas. 

Matangazo ya kibiashara

Wito huo unatolewa hivi sasa huku kukiwa hakuna muafaka wowote ambao umefikiwa baina ya Serikali na Kundi la Waasi la M23 huku mazungumzo hayo yakitarajiwa kufikia kikomo na hapa Kiongozi wa Ujumbe wa Waasi Francois Ruchogoza anabainisha.

Serikali nayo haijakaa kimya na badala yake imesema makubaliano yote yamejadiliwa hususani kile kilichoafikiwa tarehe 23 March mwaka 2009 kama anavyoeleza Francois Mwamba kutoka upande huo.

Utata umegubika mazungumzo kipindi hiki ambacho Mkutano wa ICGLR umeanza nchini DRC huku Katibu Mkuu Profesa Ntumba Luaba akisema wanajadili maeneo yote yenye mgogoro katika Ukanda huu.

Katika hatua nyingine taarifa kutoka masharki mwa nchi hiyo zinasema kuwa kuna kundi jingine ambalo limeundwa na kutambulika kama M26 kundi ambalo lenyewe halijajitanabaisha wazi litakuwa na malengo gani.