Habari RFI-Ki

Wananchi wa Gambia kufanyakazi kwa siku nne pekee na zilizosalia zitatumika kwa ajili ya Ibada na kwa shughuli za kilimo

Sauti 11:08
Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambaye ametangaza siku tatu za mapumziko nchini mwake na wafanyakazi wanapaswa kufanyakazi kwa siku nne pekee
Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambaye ametangaza siku tatu za mapumziko nchini mwake na wafanyakazi wanapaswa kufanyakazi kwa siku nne pekee

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza nchi hiyo kuwa na siku tatu za mapumziko huku wananchi wakiruhusiwa kufanya kazi kwa siku nne pekee!! hatua ya Rais Jammeh inatokana na kutaka kutoa nafasi kwa wananchi wake kutumia siku hizo kufanya ibada na kuendeleza shuguli zao za kilimo na zile za kijamii!!