Syria-oic

Viongozi wa Jumuiya Kiarabu waendelea kugawanyika kuhusu mzozo wa Syria

Viongozi wa jumuiya ya kiarabu waendelea kugawanyika kuhusu suala la mzozo wa Syria katika mkutano unaotamatika alhamisi hii jijini Cairo nchini Mirsi, wakati upande moja ukiendelea kusisitiza uungwaji wake mkono kwa serikali ya rais Bashar Al Assad huku upande mwingine ukiwaunga mkono waasi.

Matangazo ya kibiashara

Mahmoud Ahmednejad rais wa Iran mshirika wa karibu wa Utawala wa rais Bashar Al Assad katika mkutano huo ameendelea kuwatolea wito waasi kuketi kwenye meza ya mazungumzo na utawala wa Damascus na kaufikiana kuhusu kuwepo kwa uchaguzi ulio huru na wa haki, huku akisisitza kwamba raia wa Syria wenye ndio wanapashwa kuamuwa hatma ya nchi yao.

Akizungumza katika kituo cha televisheni cha nchini Misri, rais AhmedNejad amesema matakwa ya wananchi kuhusu mabadiliko, uhuru na sheria, haviwezi kupatikana kupitia njia ya vita.

Ma rais wa Misri Mohamed Morsi, Receep Tayep Erdogane katika mikutano yao ya falagha, hawakufaulu kumshawishi rais Ahmednejad kubadili msimamo wake.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Ali Akbar saleh amefahamisha kuwa Mikutano hiyo ya falagha itaendelea kufanyika katika ngazi za mawaziri wa mambo ya nje.

Upande wake msemaji wa Ikulu ya rais Yasser Ali amesema iwapo kweli Iran inataka kulinda maslahi yake katika Jumuiya ya nchi za kiarabu, inatakiwa kuisaidia Syria kukomesha machafuko ya umwagaji damu.