EU-mkutano

Viongozi wa Ulaya wakutana kujadili swala la Badgeti ya Umoja huo mwaka 2014-2020

Viongozi wa mataifa na serikali za Umoja wa Ulaya EU wanakutana leo mchana jijini Brusels nchini Ubelgiji ili kujaribu kutafuta muafaka kuhusu badgeti ya 2014-2020 baada ya kushindwa kuafikiana katika mkutano uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana kuhusu badgeti ya Umoja huo. Mazungumzo yanaonekana kuwa na utata baada ya nchi kadhaa ikiwemo Uingereza zikidai kupunguzwa kwa matumizi. Rais wa Baraza la Ulaya, Herman Van Rompuy, atawasilisha mapendeko mapya Alhamisi mchana yatayofikia maelewano. mkutano wa kilele inaendelea Ijumaa.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika moja ya mikutano
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika moja ya mikutano
Matangazo ya kibiashara

 

Rais wa Ufaransa Francois Hollande atakutana kwanza na waziri mkuu wa Italia Mario Monti na wa Uhispania Mariano Rajoy kabla ya uzinduzi rasmi wa mkutano huo. Mkutano kati ya viongozi hao watatu washirika wa jadi utajadili kuhusu sera ya kuendelea kutetea siasa ya Umoja wa Ulaya ya kutia kipao mbele kukuza ukuaji wa uchumi badala ya kupunguzwa kwa badgeti.

Jumatano jioni, rais wa Ufaransa Francois Hollande amekutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mazungumzo yao mafupi lakini yenye umuhimu. viongozi hao wawili  walionyesha nia yao ya kuona Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Ulaya wanafikia makubaliano mazuri mjini Brussels.

Hata hivyo mazungumzo hayo yanaonekana kuwa na ugumu sana kuwaleta viongozi wote 27 pamoja, kufikia maelewano, baada ya kushindwa mkutano wa kilele wa bajeti uliofanyika mwezi Novemba mwaka 2012.