Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Serikali ya Ufaransa yauomba Umoja wa Mataifa UN kupeleka Kikosi cha Kulinda Amani Kaskazini Mwa Mali huku Tanzania ikianza mchakato wa kutoa vitambulisho vya Taifa

Sauti 21:19
Wanajeshi wa Ufaransa ambao wanaendelea na operesheni zao Kaskazini mwa Mali kabla ya kuondoka na kuacha jukumu kwa majeshi ya kulinda amani
Wanajeshi wa Ufaransa ambao wanaendelea na operesheni zao Kaskazini mwa Mali kabla ya kuondoka na kuacha jukumu kwa majeshi ya kulinda amani REUTERS/Malin Palm

Serikali ya Ufaransa hatimaye imewasilisha ombi la kutaka kipelekwe Kikosi Cha Kulinda Amani Cha Umoja wa Mataifa UN kushika doria Kaskazini Mwa Mali baada ya operesheni yao ya majuma manne kusambaratisha Makundi ya Kiislam, Umoja wa Mataifa UN umeendelea kusaka mbinu madhubuti kukabiliana na machafuko yanayoshuhudiwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Maandamano makubwa yametekelezwa nchini Tunisia baada ya kukamilika kwa mazishi ya Kiongozi wa Upinzani Chokri Belaid na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa baada ya mchakato wa muda mrefu!!