Hatimaye fainali za Dimba la Mataifa Bingwa barani Afrika AFCON zimewadia na hii leo Nigeria wataumana na Burkina Faso katika kusaka kuwania ubingwa huo. Ungana na mwanamichezo wako Victor Abuso kuangazia mambo mbalimbali yanayoendelea kujiri huko nchini Afrika Kusini sambamba na maandalizi ya fainali hizo, karibu.
Vipindi vingine
-
Jukwaa la Michezo Bayern Munich mabingwa wa ligi mara ya 11 Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na maandalizi ya fainali ya kwanza kuwania taji la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania na USM Alger, ya Algeria. Vituo vya kukuza soka nchini Rwanda, vinavyofadhiliwa na klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain na Bayern Munich yashinda taji lake ya 11 katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.27/05/2023 23:55
-
Jukwaa la Michezo Dondoo ya taarifa za michezo, ikiwemo Senegal U-17 kuwa mabingwa wa Afrika. Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na ligi ya mpira wa vikapu barani Afrika kuanza leo nchini Rwanda, Yanga yatinga fainali ya kombe la shirikisho wakati Senegal watawazwa washindi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17, CAF yatangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 na orodha ya mwisho ya wachezaji watakaowania tuzo la Marc-Vivien Foe yatangazwa na RFI/France 24.20/05/2023 24:00
-
Jukwaa la Michezo Omanyala awika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic jijini Nairobi Mkenya Ferdinand Omanyala ameshinda mbio za Mita 100 katika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic yaliyofanyika jijini Nairobi, huku Mmarekani Sha'Carri Richardson naye akiibuka bingwa katika Mita 200 kwa upande wa wanawake.Tunachambua pia ligi ya soka nchini Rwanda, kufukuzia ubingwa na mchuano wa watani wa jadi nchini Kenya, kati ya Gor Mahia na AFC Leopards.13/05/2023 23:54
-
Jukwaa la Michezo Wanariadha wajipima nguvu katika mashindano ya Diamond League Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi mashindano ya riadha ya Diamond League, kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 na maendeleo ya ligi kuu za soka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.06/05/2023 23:53
-
Jukwaa la Michezo Simba SC yaondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa kombe la mataifa ya Afrika CHAN kwa vijana wasiozidi miaka 17, Simba kuondolewa kwenye mashindano ya CAF, Kenya yashinda Kombe la dunia katika mchezo wa wavu na uchambuzi wa mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania kuomba kuwa wenyeji wa michuano ya AFCON 2027.29/04/2023 23:51