MAREKANI

Rais Obama awataka wabunge kumsaidia kuinua uchumi wa Marekani

Rais wa Marekani Barrack Obama ametangaza mipango ya kuwaondoa wanajeshi wa nchi hiyo nchini Afganistan na kuinua uchumi wa taifa hilo ahadi aliyoitoa  wakati wa  hotuba ya kitaifa kwa wabunge wa Congress.

Matangazo ya kibiashara

Rais Obama alitumia hotuba hiyo kuelezea mipango yake ya miaka minne ijayo atakapokuwa madarakani kama kiongozi wa taifa hilo, katika hotuba ambayo pia alizungumzia suala la ukosefu wa ajira.

Sera ya nchi za nje nchini humo hazikuzunguziwa sana katika hotuba hiyo lakini rais Obama aliendelea kulaani serikali ya Korea Kaskazini kwa kufanya jaribio la tatu la zana zake za Nyuklia siku ya Jumanne jaribio alilosema linatishia usalama wa dunia.

Aidha, rais Obama amesema kuwa Marekani itaanza mazungumo na Umoja wa Ulaya ili kuimarisha biashara na kusaidia kuunda nafasi zaidi ya ajira kwa Wamarekani.

Obama amewataka wabunge wa Congress kuunga mkono juhudi za serikali kuinua uchumi wa nchi hiyo ambao umeonekana kudorora katika siku za hivi karibuni.

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi rais Obama amesema ikiwa wabunge hao wa Congress hawatapitisha mswada unaozuia uharibifu wa hali ya hewa hasa magari yanayotumia mafuta yanayochafua hewa.

Hotuba ya rais Obama pia iligusia namna ya kuziuia utumizi mbaya wa silaha ndogondogo kama bastola ambazo zimekuwa zikitumiwa kutekeleza mauaji ya watoto 20 wakiwa shuleni mwaka uliopita.

Uongozi wa miaka minne ijayo ya rais Obama inaangaziwa na wachambuzi wa siasa nchini humo kuona ikiwa atatekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni mwaka uliopita na kuunganisha wanasiasa nchini humo waliogawanyika.