Habari RFI-Ki

Matokeo ya Kidato cha Nne yatangazwa nchini Tanzania huku asilimia 86.62 ya wanafunzi wakianguka mtihani

Sauti 08:35
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Tanzania Dr Shukuru Jumanne Kawambwa akitangaza matokeo ya kidato cha nne
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Tanzania Dr Shukuru Jumanne Kawambwa akitangaza matokeo ya kidato cha nne

Watanzania wamekutwa na mshtuko mkubwa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Kidato cha Nne na kushuhudia asimilia 86.62 ya watahiniwa wakianguka kwenye mtihani huo. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wanafunzi kushindwa kwenye mtihani huo huku serikali kupitia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Jumanne Kawambwa akisema ukoseafu ya mahitaji muhimu kwenye shule ndiyo sababu kuu. Wananchi wengi wameshusha lawama kwa serikali na kutaka Viongozi wa Wizara kujiuzulu nyadhifa zao!!