Karibu katika Makala ya Jukwaa la Michezo na juma hili tunaangazia mgogoro wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF kuhusiana na maswala ya uchaguzi wa viongozi wa shirikisho hilo, lakini pia tutatupia macho migongano iliyochukua sura mpya katika soka la nchi hiyo baada ya kamati ya uchaguzi kumbakiza Athuman Nyamlani kuwa mgombea pekee wa Urais wa shirikisho na kuwaengua wagombewa wengine Jamal Malinzi na Michael Wambura. Ungana na mwanamichezo wako Victor Abuso upate kujua mengi zaidi kuhusiana na sakata hilo.
Vipindi vingine
-
Jukwaa la Michezo Manchester City mabingwa wa taji la FA nchini Uingereza Kocha wa klabu ya Manchester City nchini Uingereza, Pep Guardiola ameiongoza klabu yake kuishinda Manchester United mabao 2-1 katika fainali ya FA. Fainali ya pili ya shirikisho barani Afrika kati ya USM Algier na Yanga kutoka Tanzania, matukio ya riadha na Tennis ni miongoni mwa yale tuliyokuadalia kwenye Makala ya leo.03/06/2023 23:53
-
Jukwaa la Michezo Bayern Munich mabingwa wa ligi mara ya 11 Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na maandalizi ya fainali ya kwanza kuwania taji la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania na USM Alger, ya Algeria. Vituo vya kukuza soka nchini Rwanda, vinavyofadhiliwa na klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain na Bayern Munich yashinda taji lake ya 11 katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.27/05/2023 23:55
-
Jukwaa la Michezo Dondoo ya taarifa za michezo, ikiwemo Senegal U-17 kuwa mabingwa wa Afrika. Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na ligi ya mpira wa vikapu barani Afrika kuanza leo nchini Rwanda, Yanga yatinga fainali ya kombe la shirikisho wakati Senegal watawazwa washindi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17, CAF yatangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 na orodha ya mwisho ya wachezaji watakaowania tuzo la Marc-Vivien Foe yatangazwa na RFI/France 24.20/05/2023 24:00
-
Jukwaa la Michezo Omanyala awika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic jijini Nairobi Mkenya Ferdinand Omanyala ameshinda mbio za Mita 100 katika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic yaliyofanyika jijini Nairobi, huku Mmarekani Sha'Carri Richardson naye akiibuka bingwa katika Mita 200 kwa upande wa wanawake.Tunachambua pia ligi ya soka nchini Rwanda, kufukuzia ubingwa na mchuano wa watani wa jadi nchini Kenya, kati ya Gor Mahia na AFC Leopards.13/05/2023 23:54
-
Jukwaa la Michezo Wanariadha wajipima nguvu katika mashindano ya Diamond League Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi mashindano ya riadha ya Diamond League, kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 na maendeleo ya ligi kuu za soka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.06/05/2023 23:53