MALI

Rais wa Mali akanusha shutuma za jeshi lake kukiuka haki za binadamu

AFP PHOTO / HABIBOU KOUYATE

Rais wa mpito nchini Mali Dioncunda Traore ametetea vikosi vyake dhidi ya shutuma za Umoja wa Mataifa UN kuwa majeshi yake yamekuwa yakitekeleza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binauadamu dhidi ya makundi ya jamii kadhaa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Dioncunda Traore akiwa ziarani katika nchi jirani ya Senegal amesema Ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa imeeleza maswala ambayo ni nadra kufanyika lakini ameapa kuwafikisha mbele ya sheria wale wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo vya ukiukwaji wa haki za binauadamu.

Uchunguzi wa awali wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umeonesha kuwa makundi yanayolengwa na Wanajeshi wa Mali yanadaiwa kuunga mkono makundi ya watu wenye silaha na wanamgambo wa kiislamu.

Katika hatua nyingine Ufaransa imeomba jumuia ya kimataifa kufadhili shughuli za kisiasa na kijeshi nchini Mali kipindi hiki ambacho Vikosi vya ufaransa vinatazamiwa kuondoka nchini humo.