Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mbabe wa Kivita Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Jenerali Ntaganda asalimu amri wakati Umoja wa Mataifa UN ukianzisha uchunguzi juu ya matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria

Sauti 18:28
Mbabe wa Kivita kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Jenerali Bosco Ntaganda akisubiriwa kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC
Mbabe wa Kivita kutoka Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Jenerali Bosco Ntaganda akisubiriwa kupelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC REUTERS/Paul Harera

Mbabe wa Kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Jenerali Bosco Ntaganda maarufu kama The Terminator amesalimu amri na kujisalimisha katika Ubalozi wa Marekani nchini Rwanda na sasa anataraji kupelekwa katika Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC kujibu mashtaka yanayomkabili, Umoja wa Mataifa UN umeanzisha uchunguzi kubaini kama kumekuwa na matumizi ya silaha za nyuklia kwenye shambulizi lililofanyika nchini Syria katika Jiji la Aleppo na kuchangia vifo vya watu zaidi ya thelathini na Rais wa Marekani Barack Hussein Obama amefanya ziara yake ya kwanza ya kiserikali tangu achaguliwe kuongoza taifa lake kwa awamu ya pili na kuzuru Mashariki ya Kati na kuahidi atasimamia kupatikana amani ya kudumu!!